Friday, January 1, 2016

KUWA NA MAONO NA KUWEKA MALENGO.



Anza  Mwaka  2016  kwa kuandika  Mipango  Yako, ndiyo  ramani   kuu  ya   Mafanikio .

Umewahi  kujiuliza  mtu  anayetembea  njiani ,  hapajui  anakokwenda  na   hivyo   haijui   njia.Akifika  njia  panda  akamkuta  mtu , atamuuliza  “ NIFUATE  NJIA  IPI ?” Ni   lazima  naye  atamuuliza   “ UNATAKA  KWENDA  WAPI ? “  Akijibu  “Sijui”, uwe  na  uhakika     yule   anayetegemewa   kuelekeza  atajibu “ CHAGUA  NJIA  YOYOTE   UIPENDAYO  KATI  HIZI  NNE  ITAKUFIKISHA   POPOTE”. Huyu   hana  MAONO kwahiyo  ni  lazima   atajikuta  katika  matatizo  tu !  HAJITAMBUI !  Kundi  hili  ni  kubwa  sana  katika  jamii  yetu  wengi  wao  ni  wale  wasio  na  MAONO  maishani  mwao.Wanaishi  tu  kwa  hapa  na  sasa.Hawana   ndoto,malengo   wala  kitu  mbeleni. Hawajatimiza  NDOTO  zao  wala   nini , bali   wapo  tu !! Ndio  wale   husherehekea  MWAKA  MPYA  kwa  fujo  sana kwa  kuchoma   mipira, kupiga baruti , kufanya  fujo , wizi  n.k.  bila   kujiuliza  MASWALI  YA  MSINGI.
          Mtu   unapaswa   KUJITAMBUA-----WEWE  NI   NANI ? UMETOKA  WAPI ? UNAKWENDA  WAPI ?  KUFANYA   NINI ? NA  KWANINI ? UKO  WAPI ? UNAFANYA   NINI ? KWA  NINI  UNAISHI . Na  siyo   kuishi  tu  bora  upo  au  bora   liende !  HAPANA  BADILIKA  NDUGU  YANGU .




 






           Katika SAFARI  YA  MAISHA  YA   MAFANIKIO,  MAONO  NA   MALENGO    vina  nafasi   kubwa   sana katika kuwa    na mwelekeo  maalumu wa  utendaji ,bila  hivyo  hutafanya   lolote   bali   utabaki  kulalamika  kila  mwaka   unaopita  na  mwisho  wa  siku   utajikuta   hueleweki. Inakuwa  sawa    na  gari   bila   usukani. Gari  hii  haiwezi  kuekekea   mahali   kunako   takiwa,itapoteza  mwelekeo .Wakati  MAONO  yakiwa   kama   DEREVA  mwenyewe , MALENGO   kwa   upande    wake  ni  USUKANI.Hukuongoza   na   kukupeleka  unakokutaka. Ufanye  lipi   miongoni  mwa   mengine. Bila   MAONO   kasha   MALENGO  hautafanya   jambo  la  maana.
                         MAONO----DEREVA               MALENGO----USUKANI
ANGALIZO: Bila  MAONO    kisha   MALENGO  hautafanya   jambo   la   maana  ndugu  yangu.

Ndugu   yangu  kukosa  MAONO     maishani  ni   hatari.  Hata   maandiko  matakatifu ,imeandikwa  hivi ;
    “Pasipo  maono , watu  huacha  kujizuia “  Mithali  29:18a  ,   maana  yake    Pasipo  maono ,  watu  hushindwa   kujizuia  katika  mambo    yasiyofaa   kama  ulevi , wizi ,  zinaa n.k. ambapo  mwisho  wa  siku  utajikuta   matatizoni. watu  hufanya   mambo   kiholela , hawana  kitu  cha   kuwawekea  mipaka , hawana  chochote   cha   kuwasukuma  kulifuatilia  jambo    kulitekeleza   mpaka   wakalifikikisha  mwisho   wake.  Kama  hauna   MAONO  katika  maisha   yako    hata   MAISHA  yenyewe   yatakuwa  hayana  msimamo.
Kuna   msemo  wa  Kiingereza  unasema   An  idle  brain   is  the  devil    workshop”   maana  yake  AKILI  isiyojishughulisha  ni   karakana  ya  SHETANI.


Hakuna  kitu  kikubwa  hapa  duniani  kilichofanyika  bila  maono  na  shauku”. ---Georg  Wilhelm  Friedrich   Hegel.


 Watu  wengi  wanafeli  maishani  si  kwa  sababu   ya  kukosa    uwezo  au  ubongo  au  hata  UJASIRI  bali  ni   kwa   sababu  hawajakusanya  nguvu  zao  katika  MALENGO.”----Elbert  Hubbard.






MAONO  NI  NINI ?  MAONO (VISION) kwa   maneno  mengine   tunaweza  kusema   NDOTO  ni   picha  au   matazamio  anayokuwa  nayo  mtu, shirika  au  taasisi  juu  ya   ufanisi   katika    jambo   fulani.

NINI    TOFAUTI   YA   MAONO   NA   MALENGO ? Wakati  MAONO   yakiwa ni  jumla  ya   picha  ya  MAFANIKIO,  MALENGO   kwa  upande   wake  ni  kiwango/ kiasi  cha  mafanikio  ayatakayo  mtu / taasisi   ndani  ya  kipindi  fulani.  Tofauti  na  MAONO  ambayo   kwa  kawaida  huwa   hayawekwi  katika  kiwango    na  MUDA   maalumu ,  MALENGO   huwa  katika   kiwango  na  MUDA   maalum. Kwa   mfano , unapanga  kwamba  katika  kipindi   fulani  nataka  niwe  sehemu   fulani   katika  jambo   fulani.Hayo  ndiyo  MALENGO. KWA  MFANO , MALENGO  yako  yanaweza  kuwa--------“nataka  kuwa  na   magari   saba   ya  biashara  ndani  ya   miaka  mitano “.  Hapo   MAONO  ni  kuwa  na  magari (  bila  shaka  mengi tu )  ya  biashara. Lakini  MALENGO  ni  kuwa     nayo  saba   ndani  ya  miaka  mitano.


.”
  NI  HATARI  SANA   hivi   ndivyo   alivyo  mtu  ambaye  anategemewa  KUFANIKIWA  lakini   hana  DIRA /MUELEKEO----yaani  hana  MALENGO.
ANGALIZO:  Kama  huijui      NJIA  ya   unapokwenda ,  hakikisha  unayo  RAMANI  YA  NJIA   unayotakiwa  kuipita , mikononi  mwako. RAMANI   ni   dira  ya  safari .  Inaweza   kukuongoza   mpaka    mwisho   wa  safari   yako    kama  ukifuata   jinsi   inavyoelekeza  au   jinsi   ulivyoipanga WEWE   MWENYEWE. MALENGO   ni  DIRA  ya  mtu.Ni  dira  ya  huko   ankotaka  kufika. Ni  lazima  uwe  na   MALENGO  au  DIRA   kabla  hujaanza   SAFARI  YA  MAFANIKIO. Kwa  kawaida  , MALENGO  yote   huwekwa  mwanzoni   mwa  safari.
     Watu   wasipokuwa na  MAONO   kisha MALENGO , hawawezi  kuwa  na   MWELEKEO  wa  kiutendaji. Hawawezi  kujipa  NIDHAMU  YA   UTENDAJI  maana  hawana  na  hawajui  wanapokwenda. UNAFIKIRI  nini  kitawasukuma  kufanya   BIDII  ili   hali  hawajui  umbali   wanaotakiwa  kusafiri  kabla  ya   muda   fulani   na  kwa   ufanisi  kiasi  gani ?  Na  je !  Lini   watajua  wamefika  ?   Watapimaje   ufanisi   wenyewe ?

        NAMNA    YA    KUWEKA   MALENGO
Jambo  linalopelekea  wengi  wetu  kutofanikwa  ni  kukosa   kuweka  MALENGO   yanayoeleweka  na  yanayotekelezeka   kulingana   na  MAZINGIRA, MUDA,  NYENZO , n.k.
Kuna   mambo  ya   kuangalia/ kuzingatia  kabla  hujaamua  kuweka  malengo.Unapaswa  kutulia  katika  hili  kwani   hayo   ndiyo    MAISHA  yako.
Zipo  dondoo   kadhaa  katika  namna  ya  kuweka   MALENGO  ili  uweze  kupata  ufanisi  katika  SAFARI  YA  MAFANIKIO   kama  ifuatavyo :--
(1).LENGA  ENEO  NA  SHUGHULI   MAALUM. Shughuli  na  maeneo   ya  kufanikiwa  ni  mengi  mno.Mambo  ni  mengi  .Huwezi   kushughulika  na   kufanikiwa  yote.Lenga   jambo  moja   au  mawili tu.Kama  ni  biashara  basi   jikite  huko.Baadhi  ya  maeneo  ya  kufanikiwa  ni  kama  vile   Sanaa ,biashara , Michezo, Uvumbuzi  katika   teknolojia  ya   matumizi  ya   kompyuta  na  mawasiliano  ya  mtandao  n.k.
(2).WEKA   MALENGO  MAALUM  NA  YANAYOPIMIKA. Ili  uweze  kufanikiwa  vyema, unatakiwa   kuweka  MALENGO  yanayoeleweka , maalum  na  yanayopimika  kiasi  kwamba   unaweza  kwa   wakati  wowote  kupima  / kutambua  umeyafikia  na  kiasi  gani.
(3).WEKA  MALENGO  MAKUBWA    KIASI   KWAMBA   UKISHINDWA    KUYAFIKIA  BADO   UWE   UMEFANIKIWA: Hii  inasaidia  ubongo  kuwaza  sana  na   kujishughulisha   kwa  kiwango  cha  juu  zaidi  ambapo   mara  kadhaa  hupelekea  mafanikio. Utafiti  unaonyesha  kuwa  kadri   unavyopania / kulenga  jambo  kubwa  ndivyo  akili   yako   inajiweka  katika  KUFIKIRIA  na   KUTENDA  kikubwa  zaidi.
(4).WEKA   MUDA   MAALUMU  KATIKA    MALENGO  YAKO: Kumbuka   kuwa  MALENGO  huenda  na   MUDA. Bila   kujiwekea  MUDA   hautapata   msukumo  wa  kutenda  kwa  WAKATI. Pasipo  na   MUDA   hautaweza  kujitathmini---kuona  nini    umekifanya /  kukipata  katika  kipindi   Fulani. Kuweka    MALENGO  YA   MUDA  MREFU  na   MALENGO  YA   MUDA  MFUPI  kama  mwaka  mmoja. JIPANGIE   MUDA , JIBANE  na   JISIMAMIE   WEWE  MWENYEWE.
 
 

SIFA  ZA  MALENGO    MAZURI
----Lengo  ni  lazima  liwe   MAALUM  na liwe  linaelezeka. Mfano  lengo  la  kuwa  daktari  bingwa  wa  watoto.
----Lengo  lililowekwa   vizuri  siku  zote  huwa  LINAPIMIKA.
---Lengo   zuri   lazima  liwe   LINATEKELEZEKA.
----Lengo  lazima   liwe   LINAFIKIKA.
-----Lengo  zuri  ni    lazima  liwekewe   MUDA  wa  utekelezaji.



VISION—An  idea  or   picture  in   your   imagination.
GOAL---Something  that  you  hope  to  achieve.

 Makala  hii  imeandikwa  na  MWL   JAPHET   MASATU , Mwandishi, mwelimishaji, , mhamasishaji   katika   masuala  ya kimafanikio, ujasiriamali ,biashara  na  mambo  ya  kimaisha kwa  ujumla .Anapatikana  kwa  namba  :  Call /  WhatsApp +255 755 400 128 /  +255 716 924 136.  E-MAIL :  japhetmasatu@gmail.com.
01/01/ 2016 Ijumaa.