Kila siku unayoianza, ainisha mambo matano muhimu ambayo ukiyafanya
siku hiyo yatakusogeza karibu na mafanikio unayotaka kuyafikia. Mambo
hayo matano unapaswa kuyafanyia kazi bila ya kujali mazingira yapoje.
Inyeshe mvua au liwake jua, hayo matano ni muhimu kwa siku yako na
unapaswa kuyafanyia kazi.
Kwa kuwa na tano za siku, unajiweka kwenye nafasi ya kutekeleza yale
muhimu na kuepuka kupotezwa na kelele ambazo zimekuzunguka kila mahali.
No comments:
Post a Comment