HISIA NI NINI ? Kuna tofauti gani kati ya HISIA na MATAMANIO ?
BINADAMU ana NAFSI MBILI. Nafsi ya kumuelekeza MAZURI na Nafsi ya kumuelekeza MABAYA.
KWA MFANO , unaweza kuwa unataka kutenda JAMBO BAYA. Bila shaka kuna sauti nafsini kwako inakunong"oneza , USIFANYE JAMBO HILI , nyingine inakwambia FANYA ! Inayokwambia "USIFANYE NI HISIA " inayokwambia " FANYA" ni MATAMANIO.
Bila shaka umewahi kusikia MTU akimwambia mwenzake , " UNA MACHALE SANA , VINGINEVYO UNGEIBIWA ! " Je, unafikiri hii inamaanisha NINI ? Hii ni " HISIA " ndiyo iliyomwongoza na kumwepusha na balaa la kuibiwa .
AU unaweza kuwa umezungukwa na watu , unasikia SAUTI INAKUNONG"ONEZA , " KIMBIA HARAKA ! Hawa watu ni HATARI kwako. " Lakini sauti hiyo haiwezi kusikika kwa mtu mwingine yeyote zaidi yako. JE , UNAFIKIRI HUYU ANAYEKUNONG"ONEZA NI NANI ? NI " HISIA " NDIYO INAYOONGEA NA WEWE ! Watu wengi hudharau "HISIA" zao na mwishowe hupata MATATIZO.
KILA MTU ANA HISIA. Watu hutumia lugha: " CHALE ZILIMCHEZA ", wakimaanisha : " HISIA ZILIMWAMBIA."
HISIA ni NGUVU iliyo ndani ya mwili wako ambayo HUKUONGOZA. Zimewekwa katika mwili wako kwa malengo maalumu KUKUSAIDIA. PINDI unapotawaliwa na MATAMANIO , ni hakika kwamba baadaye UTAWEZA KUKOSA FURAHA. HISIA hujaribu KUKUTAARIFU kuwa JAMBO FULANI SI ZURI . HUKUSISITIZA ZAIDI NA ZAIDI.
UKIONA HISIA zinakuzuia KUFANYA JAMBO , LIACHE MARA MOJA. KISHA , TOKA UTAFAKARI AU UWAULIZE WENGINE. Kwa kufnya hivyo , itakusaidia KUPAMBANUA MWELEKEO WA HISIA ZAKO.WANAOHESHIMU HISIA ZAO HAWAJUTI.
ANZA KUHESHIMU HISIA ZAKO , si kwamba UTAPATA PESA TU , BALI kuna mambo mengi ambayo UTAWEZA KUFANIKIWA MAISHANI KUTOKANA NA KUHESHIMU HISIA ZAKO.
HISIA zinavutia. WAPELELEZI hutumia HISIA. HISIA Zinapowambia JAMBO HUSIMAMA. HUZISIKILIZA. kisha huzifanyia kazi.Vivyo hivyo , hata WANASAYANSI , WATABIRI ,MADAKTARI N.K.
KILA SIKU HISIA ZINAZUNGUMZA NA SISI . KINACHOTAKIWA NI KUZIHESHIMU.
HISIA NI KIONGOZI NA MSHAURI WETU TUMHESHIMU ILI TUEPUKANE NA MATATIZO MBALIMBALI.
No comments:
Post a Comment