Huu ndiyo wakati mzuri kwako mfanyabiashara kuwaonesha wateja
waaminifu kwako kwamba biashara yako inawajali, haiangalii tu kuingiza
faida, bali inataka mteja aendelee kuwepo.
Kuna baadhi ya wateja wako watakuwa wamekwama kutokana na hali
inavyoendelea, iwapo watakueleza kukwama kwao na ukawa na njia ya
kuwasaidia, wafanya hivyo. Kwa sababu usipowasaidia na wao wakashindwa,
basi biashara yako itakuwa imepoteza mteja moja kwa moja.
Mfano; kama kuna wateja umekuwa nao kwa muda mrefu
na wamekuwa walipaji wazuri bila kusumbua, ila kipindi hiki wameshindwa
kulipa kwa wakati, wape nafasi ya kuchelewa kulipa au kulipa kwa viwango
tofauti na awali kama ipo ndani ya uwezo wako.
No comments:
Post a Comment