BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE. JIFUNZE ---ELIMIKA --CHUKUA HATUA---FANIKIWA
Tuesday, May 27, 2025
Thursday, May 22, 2025
MAKALA : MAISHA SI BAHATI NASIBU AU KUBET . NI RAMANNI YA MABADILIKO NA DIRA . NI MAAMUZI NA MAANDALIZI------NA MWL. JAPHET MASATU------TANZANIA -------FRIKA YA MASHARIKI--------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Kakaa/Dadaa....
Unajua shida kubwa inayowakumba wengi?
Wanaamka kila siku…
Wanakimbizana kama mchwa waliomwagiwa maji…
Lakini hawajui wanakimbilia wapi.
Kila siku ni kujituma…
Lakini mwisho wa mwezi, mfuko ni kama shimo la panya.
Kila mwaka unakatika…
Lakini hakuna mabadiliko ya maana.
Wengi wako kwenye 'autopilot' ya maisha.
Wanajisukuma tu.
Wakiamini ipo siku mambo yatajileta.
Mambo hayajileti. Wewe ndo lazima uyasogeze.
Hii Inatisha Kidogo…
Unaamka ukiwa na nguvu.
Unaota mafanikio.
Lakini kila jioni, unarudi na uchovu tu.
No progress.
No peace of mind.
Unasema utabadilika kesho.
Kesho ikifika, unafanya yaleyale.
Ni kama umefungwa pingu zisizoonekana.
Hii ni hatari sana.
Inaua ndoto zako taratibu bila kelele.
Alafu unakuja kushangaa:
“Mbona maisha yananizunguka?”
Ni kwa sababu hakuna mwongozo.
Kuna Uongo Mmoja Mkubwa…
Eti “kuwa na bidii, utafanikiwa.”
Wongo huo.
Watu wengi wana bidii kuliko hata gari la kubeba mawe.
Lakini wako pale pale.
Tatizo si bidii.
Tatizo ni kutokuwa na DIRA.
Hakuna ramani.
Hakuna mwongozo.
Na kama hujui unakokwenda…
Hutajua hata ukifika.
Sasa Sikiliza Vizuri…
Maisha yako yanahitaji mfumo.
Mfumo wa kuweka malengo.
Kujijua wewe ni nani.
Unataka nini.
Na kwa nini unakitaka.
Halafu?
Anza kupanga hatua ndogo ndogo.
Kila siku.
Kidogo kidogo hadi kikamilike.
Na muhimu zaidi, tafuta maarifa ya kweli.
Si porojo.
Maarifa ya watu waliopitia moto.
Walioungua.
Wakaamka.
Wakasimama tena.
Ngoja Nikupe Kisa Cha Huyu Bwana Mdogo Hapa…
Kuna Bwana Mdogo mmoja mtaani kwetu Anaitwa Baba T.
Miaka mitano iliyopita alikuwa anauza vocha na peremende stendi.
Maskini alikua anavaa viatu vilivyochanika…
Watu walimcheka.
Lakini kuna siku moja aliniambia:
“Bro, nimeshaamua. Sitaki kufa maskini. Nataka mafanikio ya ukweli.”
Akanunua daftari.
Akaandika malengo yake.
Akasoma vitabu.
Akatafuta mentor.
Akaanza kuandika kila kitu anachotumia.
Leo hii?
Ana duka lake la simu.
Anauza online.
Anatoa ushauri kwa vijana wengine.
Na bado ni yule yule – Baba T ila mwenye mwongozo mpya wa maisha.
Na Wewe Unaweza Kubadilika Leo…
Ukiamua, unaweza.
Ukiwa na mwongozo sahihi, maisha yanabadilika.
Unapunguza makosa.
Unafupisha safari ya mateso.
Unapanda ngazi haraka.
Chukua hatua.
Andika malengo yako.
Soma kila siku.
Tafuta watu wanaojua kuliko wewe.
Achana na kelele za mtaani.
Focus.
Maisha ni yako.
Na hakuna atakayeyaishi kwa niaba yako.
Unataka mafanikio ya kweli?
Tafuta mwongozo.
Fuata mfumo.
Jitahidi bila kusahau mwelekeo.
Maisha si bahati.
Ni maamuzi na maandalizi.
ENDELEA KUSOMA HAPA UTAPATA RAMANI YA MABADILIKO NA DIRA YA MAISHA YAKO.
Sunday, May 18, 2025
MAKALA : NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA NA NDOTO ZAKO UMEIBEBA WEWE MWENYEWE NA SI MTU MWINGINE--------NA MWL. JAPHET MASATU -------CALL / SMS / WHATSAPP + 266 716 924 136
Kakaa/Dadaa Yangu...
Umesahau wewe ni nani.
Umesahau kuwa ndani yako kuna nguvu ya kutikisa dunia.
Umejikatia tamaa kimya kimya.
Kila siku unasema *labda mimi sina bahati.*
Umeanza kuamini maisha ni magumu na huwezi kubadilisha chochote.
Lakini ukweli ni huu: UNA NGUVU YA MIUJIZA NDANI YAKO ,
Unaitumia vibaya.
Au hujui hata ipo.
Ulishawahi kumuona mtu aliyeanzisha biashara kwa buku 5 akafika juu?
Ulishawahi kumuona mtu aliyefeli shule lakini leo anaajiri waliopata division one?
Ulishawahi kumuona mtu aliyetelekezwa, akasota, lakini leo anajenga nyumba yake?
Wote hawa hawakuwa na miujiza ya mbinguni.
Walitumia nguvu ya ndani waliyoamka nayo kila siku.
Na hiyo nguvu wewe pia unayo.
Lakini... unaitumia kuskroll TikTok.
Unaitumia kulalamika.
Unaitumia kutafuta huruma badala ya suluhisho.
Una nguvu lakini hauna mwelekeo.
Miujiza sio kupasuliwa mbingu.
Sio malaika kushuka.
Miujiza ni pale mtu wa kawaida anapoamua kuamka na kuchukua hatua isiyo ya kawaida.
Ni pale mtu anapoamua kuamka kabla ya wengine.
Kuanza kuandika ndoto zake.
Kuanza kusoma vitabu badala ya magazeti ya udaku.
Kuanza kuomba kazi kwa bidii badala ya kuomba msaada.
Miujiza ni matokeo ya msimamo.
Suluhisho Lipo. Na Lipo Ndani Yako.
Badilisha namna unavyofikiri.
Acha kusema “sina mtaji” sema “naanza na hiki kidogo.”
Acha kusema “nimechelewa” sema “leo ndiyo siku yangu ya kwanza.”
Acha kujificha nyuma ya visingizio.
Toka uvunguni.
Toka kwenye comfort zone ya umaskini wa mawazo.
Chukua hatua.
Anza leo.
Fanya kitu.
Kwa sababu NGUVU YA MIUJIZA UMEIBEBEA WEWE MWENYEWE.
Bado namkumbuka....
Kuna bro mmoja alichoka na maisha.
Alikuwa hana kazi. Hana mtaji. Hana cheti.
Alikaa chini akaandika: “Mwaka huu lazima niwe mtu mwingine.”
Akaanza kuuza karanga mtaani.
Akaweka akiba ya mia mia.
Alikuwa anasoma vitabu alivyokopeshwa.
Alifungua YouTube kujifunza marketing.
Miaka mitatu baadaye...
Ana biashara ya kuuza nafaka.
Ana familia.
Ana ndoto mpya kila mwaka.
Aliniambia hivi:
“Miujiza haikunitokea, niliitengeneza mwenyewe.”
Sasa Wewe Una Sababu Gani Ya Kukata Tamaa?
Huna sababu.
Una kila sababu ya kusimama.
Chukua kalamu na kuandika ndoto zako.
Zima data saa tatu usiku na kupanga kesho yako.
Na anza kutenda miujiza ya kweli kupitia nguvu yako ya ndani.
Kumbuka: Miujiza Haiporomoki.
Miujiza hutengenezwa.
Na hutengenezwa na watu kama wewe.
Watu wa kawaida lakini walioamua kuishi maisha ya ajabu.
ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII UTAJIFUNZA MENGI " MAISHA NA MAFANIKIO ( LIFE & YOU ) BLOG " PENDA KUNUNUA VITABU NA KUVISOMA UTAGUNDUA SIRI NYINGI ZA DUNIA HII.